![]() |
Ulugu sahani, the nomad Wasukuma ni kabila kubwa zaidi nchini Tanzania : |
linakadiriwa kufikia watu milioni 7, idadi inayowakilisha asilimia 16 ya wakazi wa nchi kwa ujumla.
Jina "Wasukuma" lina maana ya watu wa upande wa " kaskazini ", lakini maana hii haiwakilishi maana halisi ambayo watu wengi huitafsiri kwa mfano Wasukuma
hutumia alama ya utambulisho (dira ) kwa eneo fulani kwa
viashirio vya makabila, kwa mfano wa jina kama hili:
Kiya. Hili lina maana ya mashariki ambako ni maawio ya jua. Huu
ni utambulisho ambao haukufananishwa ama kuitwa kwa
jina la kabila fulani. Mfano mwingine ni upande wa
"Dakama" ambapo yatambulisha kama eneo la Unyamwezi
lakini zaidi ya mpanuko wake ni upande wa "kusini". Zaidi
ya hapo neno hili hutumiwa sana na kabila la Wanyamwezi
ili kutambulisha eneo la Wasukuma ambapo Wasukuma
nao husema "dakama". Upande mwingine ambao unapewa
alama ya utambulisho ni "Ushashi" maana yake ni upande
wa kabila la Washashi na neno hili Washashi ni
mkusanyiko wa makabila ya mkoa wa mara , japo pia neno
hili "shahi" linamaanisha kabila la Wakurya ambalo pia
mpanuko wake unakomea hapo, ambapo zaidi ya hapo
eneo zima la upande huo unamaanisha upande wa
kaskazini. Upande wa mwisho kutambulishwa ni "Ngw’eli",
neno hili halikupewa kabila na badala yake linawakilisha
upande wa magharibi (dira), ambako ni machweo ya jua.
"Wasukuma wenyewe hulirejea jina hili kama "Basuguma"
kwa wingi na "Nsuguma" kwa umoja.
Eneo
Wasukuma huishi eneo la kaskazini magharibi mwa Tanzania, karibu na mwambao wa kusini mwa Ziwa Victoria , na maeneo mbalimbali ya utawala ya wilaya ya
Nyamagana, Mkoa wa Mwanza , upo pia kusini magharibi
mwa mkoa wa Mkoa wa Mara , Mkoa wa Simiyu na Mkoa
wa Shinyanga.
Eneo la kaskazini la makazi yao ni katika mbuga maarufu
Serengeti . Familia za Wasukuma wengi sana wamehamia
maeneo ya kusini kuelekea mkoa wa Rukwa ambao baadae
umegawanywa na kuzaa mkoa wa Katavi, wakipita maeneo
ya kabila la Wapimbwe na hivyo kufanya makazi katika
eneo hili la kijiji cha Wapimbwe.
Eneo hili linakadiriwa kuwa na ukubwa wa mita za mraba
910 hadi 1200.
Mwinuko wake unakadiriwa kuwa inchi 20 hadi 40 ya ujazo
wa mvua kutoka Novemba hadi Machi.
Kiwango cha juu cha joto hutegemea angalau ni kutoka
wakati kiwango cha chini nyakati za usiku hushuka na
kufikia 15°C.
Maeneo yaliyo na madini
Wasukuma wamezungukwa na madini mbalimbali.
Yafuatayo ni maeneo yaliyo na madini: 1. Mwadui (Huku
kuna madini ya almasi ambayo kwa kiwango kikubwa
huipatia serikali pesa za kigeni) 2. Maganzo (Vilevile eneo
hili limewekwa kwa ajili ya wachimbaji wadogowadogo wa
almasi, eneo hili liko magharibi ya Mwadui.)
Shughuli za kiuchumi
Shughuli kuu za kiuchumi kwa Wasukuma ni kilimo, uvuvi,
ufugaji na biashara.
Pamba ndio zao kuu la kibiashara kwa wasukuma, ambao
pia hulima mazao mengine kama mpunga, tumbaku,
mahindi, viazi , dengu na ma tunda ( kisiwani Ukerewe )
Wasukuma pia ni wafanyabiashara na uvuvi, madini
mbalimbali kama vile dhahabu, almasi na madini
mengineyo ambayo huchimbwa katika maeneo mbalimbali
mikoa ya Mwanza na Shinyanga.
Wasukuma pia wanajihusisha sana na kilimo cha mazao ya nafaka na mifugo ya aina mbalimbali. Maeneo ya Shinyanga wanalima mazao ya nafaka kama mahindi na
mpunga. Idadi ya watu inaongezeka kwa kasi na hivyo pia kuongezeka kwa wakulima wa mbogamboga .
Shughuli za sherehe
Wasukuma wengi katika karne ya 20 walitumia utamaduni
wao zaidi katika kusherehekea matukio ya nyakati
mbalimbali, kwa mfano wakati wa mavuno, unyago , ndoa ,
misiba n.k.
Watemi ndio walikuwa viongozi wa kabila la Wasukuma na
watu walikaa kiukoo katika eneo moja.
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu .
Je, unajua kitu kuhusu Wasukuma kama historia
yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza
au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na
kuongeza habari .
No comments:
Post a Comment